Idara ya Usafiri na Leseni

IDARA YA USAFIRI NA LESENI.

1.0 Utangulizi

Baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 1964 huduma za usafiri na mawasilino zilikuwa chini ya iliyokuwa Wizara ya Kazi, Ufundi, Njia na Simu. Kwa nyakati tofauti shughuli za sekta ya usafiri na mawasiliano zilikuwa zikijumuishwa pamoja na sekta nyengine kama vile ujenzi, ufundi na nyenginezo..

Mwaka 1978 ilibadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ambayo ilidumu hadi mwaka 2010 ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na mwaka 2016 ikabadilishwa tena jina na kuitwa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji.

Idara ya Usafiri na Leseni ilianzishwa mwezi Juni mwaka 2001 chini ya iliokuwa Wizara ya Mawasilisno na Uchukuzi ikifanya kazi kwa kutumia sheria iliorithiwa kutoka kwa wakoloni ijulikanayo kama ‘Road Traffic Decree cap 35’. Idara ilianzishwa kwa lengo la kusimamia shughuli zote za usafiri wa barabarani katika visiwa vya Unguja na Pemba, Kusimamia Bohari kuu za serikali Unguja na Pemba pamoja na kuendesha Karakana Kuu na sehemu za mitambo ziliopo Malindi Unguja na Cahake chake Pemba.

Mwaka ( 2003) Sheria nambari 7 ya Usafiri barabarani ilipitishwa rasmi ilioipa mamlaka Idara ya Usafiri na Leseni kutekeleza majukumu yake yanayohusiana na usafiri wa barabarani katika visiwa vya Zanzibar.

1.1 SEHEMU ZA IDARA

Idara ya Usafiri na Leseni imegawika katika sehemu zifuatazo:-

 • Ofisi kuu ya Idara iliyopo Mwanakwerekwe.
 • Sehemu ya Karakana kuu iliyopo Chumbuni.
 • Sehemu ya Upasishaji wa vyombo vya moto iliopo Karakana.
 • Sehemu ya Idara iliyoko Chakechake Pemba.

1.2     MAJUKUMU YA IDARA

Majukumu makubwa ya Idara hii ni haya yafuatayo:-

 • Kusimamia Sekta ya Usafiri barabarani.
 • Kukagua na kupasisha vyombo vya moto vinavyotumia barabara.
 • Kuwafanyia majaribio ya nadharia na vitendo madereva wanafunzi.
 • Kutoa leseni kwa madereva wanafunzi, vyuo vya udereva, walimu wa skuli za udereva
 • Kutoa leseni kwa magari ya biashara.
 • Kutoa ruhusa za njia na usafirishaji.
 • Kutoa beji za Utingo na Madereva
 • Kutoa vibali kwa magari na wageni wanaoendesha Zanzibar.
 • Kuendesha na kusimamia karakana kuu ya Serikali iliyoko Chumbuni na sehemu ya mitambo iliyoko Pemba.
 • Kusimamia shuhuli za Bodi ya Usafiri Barabarani na Kamati ya Kitaifa ya wiki ya Usalama Barabarani.

1.2.1. UTOAJI WA LESENI ZA KUENDESHA VYOMBO.

Muombaji wa leseni ya kujifundishia chombo cha moto anatakiwa kupitia hatua tatu ili kupata leseni ya kuendesha chombo.

(i) Kukata leseni ya kujifundishia(leaner’s license, ili kupata leseni ya kujifundishia muombaji anatakiwa kuwasilisha maombi ya kupatiwa leseni ya kujifundishia (Learner’s Lisence)baada ya kufanya mambo yafuatayo:-

 • Kujiunga na Chuo cha Udereva ili kupata mafunzo ya kuendesha chombo.
 • Kufanya uchunguzi wa afya yake katika Hospitali za Serikali. Kuwasilisha picha mbili ‘‘passport size’’ ambazo hajavaa kofia kwa mwanamme na awe hajavaa nikab (hajafunika uso) kwa mwanamke.
 • Kopi ya kitambulisho cha Mzanzibari/Passpoti au Cheti cha kuzaliwa.

(ii) MITIHANI YA NADHARIA.

Hatua ya pili kwa muombaji wa leseni baada ya kupata leseni ya kujifundishia (Learner’s lisence) ni kufanya mitihani ya nadharia ambayo imegawika sehemu mbili:

(i) Alama za barabarani (Road signs and symbols).

(ii) Sheria za barabarani.

Kila mtahiniwa analazimika kulipia na kufanya mitihani na kupata alama sabiini(70%) kila sehemu ili kuendelea na hatua ya kufanya mitihani ya vitendo (Practical driving test).

Iwapo mtahiniwa hakupata alama 70% sehemu moja au zote mbili atalazimika kuerejea mtihani aliokosa alama 70.

 (iii) MITIHANI YA VITENDO.

Mtihani wa vitendo ni hatua ambayo muombaji wa leseni hujaribiwa kwa vitendo uelewa wake wa sheria na alama za barabarani, mtahiniwa huyo hutakiwa kulipia mtihani wa vitendo, na kufanyiwa mambo yafuatayo:-

 • Kujaribiwa uwezo wake wa kuona kabla ya kuanza majaribio ya kuendesha chombo (visual test).
 • Kufanyiwa mtihani wa awali (Pre test) kuangalia iwapo gari anayotaka kufanyiwa majaribio inafaa kwa shughuli hiyo.
 • Kufanyiwa mtihani wa kuendesha ndani (indoor test)
 • Kufanyiwa mtihani wa nje (out door test)

Iwapo Mkaguzi amethibitisha kuwa mtahiniwa anaelewa vyema sheria na alama za barabarani kwa kupata alama 70 au zaidi humpatia cheti cha matokeo (statement of results) kinachotumika kutayarishia cheti cha umahiri (Certificate of competence) ambacho kitatumika kutengenezea leseni kulingana na daraja aliloomba.  

1.2.2. UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO.

Idara ya Usafiri na Leseni inafanya ukaguzi wa vyombo va moto vinavyotumia barabara ili kuangalia uzima wa vyombo, ukaguzi huo uko wa aina nne.

 1. Ukaguzi wa mwaka (Annual inspection)
 2. Ukaguzi wa ajali
 3. Ukaguzi wa shaka.
 4. Ukaguzi maalum

Ukaguzi wa mwaka: Ukaguzi huu hufanyika kwa kila chombo cha moto kinaoptaka kuingia barabarani na kinapofikia mwaka tokea kilipopasishwa awali, ukaguzi huu unafanyika ili kuweza kuangalia uzima wa chombo kutokana kutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ukaguzi wa ajali: Ukaguzi huu hufanyika kila inapotokea ajali ili kubaini uzima wa chombo na chanzo cha ajali iliyotokana na chombo husika pamoja na kuangalia leseni ya dereva.

Ukaguzi wa shaka: Ukaguzi huu hufanyika muda wowote ikitokea chombo cha moto kuhusiana na kimetiliwa mashaka uzima wake, chombo hicho huchukuliwa na kupelekwa kwa mkaguzi ili kikaguliwe iwapo kinafaa kutembea barabarani au hakifai.

Ukaguzi wa maalum: Ukaguzi huu hufanyika muda wowote inapoonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kuangalia mambo mbali mbali yanayohusu taratibu za usafiri wa barabarani, kama kuangalia hati mbali mbali za kufanyia biashara ya kusafirisha abiria na mizigo pamoja na uzima wa vyombo.

1.2.3. LESENI ZA MAGARI YA BIASHARA    

Idara ya Usafiri na Leseni inatoa leseni za magari ya biashara ya aina nane kama zifuatazo:-

 1. Daladala (Town bus)
 2. Shamba (Stage bus)
 3. Private hire
 4. Magari ya wafanyakazi
 5. Magari ya wanafunzi
 6. Taxi
 7. Magari ya kukodisha na kuendesha mwenyewe (Hire and Drive)
 8. Mizigo A na Mizigo C ( Mizigo A gari za biashara na Mizigo C ya nyumbani).

Muombaji wa leseni ya gari ya biashara anatakiwa kufanya mambo yafuatayo ili kupatiwa leseni hiyo:-

Gari liwe limepasishwa.

Gari liwe limekatiwa bima.

Gari liwe linajuilikana katika halmashauri husika (kwa daladala na shamba).

Gari likatiwe leseni ya njia (road lisence)

1.2.4.UTOAJI WA VIBALI KWA MADEREVA WENYE LESENI ZA KIGENI

Wageni wanaohitaji kuendesha vyombo vya moto Zanzibar ambao nchi zao zimeridhia mkataba wa Geneva wa mwaka 1949 na Viena wa mwaka 1968 leseni zao zinatambuliwa na hupewa vibali vya utambulisho kuendesha vyombo Zanzibar.

Mhusika kutakiwa kuwasilisha leseni yake ili kuthibitishwa (verification) kabla ya kupewa kibali.

1.2.5.BEJI ZA UTINGO NA MADEREVA

Idara ya Usafiri na Leseni inasimamia watoaji wa huduma za usafirishaji wa abiria kwa kuwapatia beji Utingo na Madereva. Dereva hutakiwa kujaza mkataba maalum wa utoaji wa huduma hiyo, kuwasilisha kopi ya leseni yake, kitambulisho cha Mzanzibari pamoja na picha mbili ‘pasport’ size.

Utingo hutakiwa kujaza mkataba kuwasilisha kitambulisho cha Mzanzibari pamoja na picha mbili ‘’passport size’’.

 1.2.5. SEHEMU YA KARAKANA

Karakana Kuu ya Serikali na sehemu ya Mitambo ilioko Pemba zinahusika na utengenezaji wa vyombo vya moto vya watu binafsi na Serikali.

Kazi zinazotekelezwa Karakana Kuu ni kama zifuatazo:-

 1. ‘‘Injection section’’, sehemu hii inahusika na kurekebisha, kubadilisha na

         kuzifanyia marekebisho injector pumps pamoja na nozzle.

 1. ‘‘Service section’’, hii ni sehemu inayohusika na kuzifanyia matengenezo ya utunzaji, umwagaji wa oil, maji ya betri, engine oil, diesel na petrol filer, gear oil na kadhalika ili kuondoa vifaa ambavyo vinaweza kuharibika mwenendo wa chombo.
 1. ‘‘Engine maintenance and repair’’, sehemu hii inahusika na kutengeneza mashine zenye matatizo ya aina mbalimbali

      4. Unyooshaji na utiaji wa rangi, hii ni sehemu ambayo gari lililoathiriwa kama kupata ajali hunyooshwa na kutiwa rangi ili kurejea hali ya kupendeza.