Ujenzi wa Barabara chake chake- Wete
18-03-2022 16:03:34
Habari zilizopo
Fungua ZoteSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kuzijenga barabara zote zinazoenda katika maeneo ya utalii Nungwi na Kendwa kutokana na sekta hiyo kuchaingia sehemu kubwa katika uchumi wa Zanzibar. Viongozi wa wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Shomar Omar Shomar kwa kushirikiana viongozi wa Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) chini yausimamizi wa Meneja miundombinu-PDB Mhandisi John Msemo wameeleza hayo wakati walipofanya ziara ya kuzikagua barabara mbali mbali zilizipo katika eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wamebainisha kwamba,Kilomita 12.5 za barabara zinazotoa huduma katika maeneo ya utalii zitajengwa katika eneo la Nungwi ili kuondoa changamoto inayowakabili wananchi na wawekezaji wa hoteli katika maeneo hayo. Wamesema Serikali itaanza kuzijenga barabara zinazoendea katika hotel ya Zalu pamoja na barabara inayoendea katika eneo la uwanja wa ndege wa Nungwi zikifuatiwa na barabara nyengine. Wamefafanua kuwa Serikali itaanza na barabara hizo kutoka na urahisi wake huku Serikali ikiendelea kufanya tathmini kwa barabara zilizokuwepo katika maeneo ya makaazi ya wananchi ili kuona namna bora ya kuweza kuyaondosha maji kwa kujenga misingi ya kupititishia maji. Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini wamesema wanafuatilia kwa karibu utekelezaji kutokana na agizo la Mhe. Rais ameshatoa maelekezo ya kujengwa barabara zote zinazokwenda katika maeneo ya utalii katika kiwango bora kwa kuziwekea misingi ya kupitishia maji. Akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa barabara hizo Injinia kutoka kapuni ta URKUN Iddy Habibu Mbarouk amesema kapuni inaangalia uwezekano wa kuandaa na kurekebisha michoro na kuiwasilisha sehemu husika. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara hizo na Kampuni ya URKUN ikizijumuisha na barabara ya Jumbi - Tunguu, barabara ya Charawe- Ukongoroni- Bwejuu pamoja na barabara ya Bungi ambayo ujenzi wake umekamilika.
Watendaji wa taasisi za Serikali zinazohusiana na masuala ya miundombinu wametakiwa kuchukua hatua katika kuhakikisha miradi ya miundombinu inakamilika kwa wakati uliopangwa. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ametoa wito huo wakati akifungua kikao cha wadau wa ujenzi wa barabara za mjini 100.9km zinazotarajiwa kujengwa hivi karibuni. Amesema wadau wa sekta wanapaswa kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha harakati za ujenzi zinaendelea lakini pia wahakikishe na huduma za kijamii zinaendelea kupatikana kama vile maji, umeme na mawasiliano kwa wananchi. Waziri Dk. Khalid amewataka wahusika wanaousika na masuala ya fidia kuwa waangalifu wakati wa kufanya tathmini ya fidia ili kuepusha udanganyifu. Katika kulipatia ufumbuzi suala hilo Dk. Khalid amewataka watendaji hao wakati wakifanya zoezi hilo wachukue picha za walengwa na mali zao wakati wakiwa katika maeneo yao halisi. Akizungumzia juu ya suala la fidia Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Ndugu Khadija Khamis Rajabu amesema kumekuwa kukijitokeza changamoto kwa Serikali ya kuwalipa watu fidia zisizokuwa na msingi kutokana na baadhi ya watu kujenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara jambo linaiweka wizara katika wakati mgumu. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amepongeza jititihada za wizara ya ujenzi kwa kuitishia kikao hicho cha wadau kwani kufanya hivyo kunasaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha watendaji wote wanakuwa na mtazamo wa pamoja juu ya mradi uaotekelezwa. Akifunga kikao hicho Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Nadir Abdula-tif Yussuf amewataka baadhi ya watendaji kuanza kuchukua hatua kabisa ya kundosha miundombinu sehemu ambazo miradi ya barabara itapita ili kuwaondoshea usumbufu wajenzi waliopewa kazi ya ujenzi wa barabara hizo.
Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar umefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya bara bara zinazokwenda katika miradi ya spitali zinazoendelea kujengwa kwa lengo la kuimarisha miundombinu hiyo. Viongozi hao wa wizara wamefanya ziara katika spital zinazojengwa za wilaya na kwa barabara zinazokwenda katika majengo ya maendeleo ikiwemo spital, skuli zizopo Jango’mbe kwa bint Amrani, Mwanakwerekwe, Chumbuni, na kumalizia katika eneo Lumumba. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed amesema Serikali kupitia wizara ya ujenzi itazijenga barabara hizo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya serikali kuimarisha mifumo ya barabara. “Niseme tu miradi yote iliojengwa kwa fedha za ahuweni ya UVIKO 19 tutahakikisha tunafikisha miundombinu ya barabara kwa lengo la kuweka haiba nzuri katika majengo hayo” Alisema waziri Dk. Khalid Aidha, Mhe. Waziri amesema zipo baadhi ya barabara zitanjgwa na Wakala wa barabara Zanzibar na barabara nyengine zitajengwa na kampuni ya CCECC kutoka nchini China.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameutaka uongozi wa Shehia ya Kandwi kutoa ushirikiano kwa Serikali juu upatikanaji wa rasilimali ya kokoto na kifusi kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinazotarajiwa kujengwa. Waziri Dk. Khalid ameeleza hayo akiwa katika ziara maalum ya kukagua na kuzungumza na wananchi wa Shehia ya Kandwi Wilaya wa Kaskazini "A"Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo katika ziara hiyo Waziri Dk. Khalid ameambatana na Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Nadir Abdula-tif Yussuf. Mhe. Waziri ameutaka uongozi wa shehia ya Kandwi pamoja na wananchi kutoa ushirikiano wao kwa wakandarasi wa Kapuni ya CCECC ambao watalitumia eneo hilo kwa ajili ya kupata rasilimali kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali Kupitia wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi itahakikisha inasimamia kwa karibu juu ya upatikanaji wa haki ya fidia kwa wananchi ambao maneo yao yatatumika kwa ajili ya kazi ya uchimbaji wa rasilimali. "Nawahakikishia kuwa hakuna mawananchi hata mmoja atakaedhulumiwa, lakini pia Mhe. Sheha hakikisha hakuna udanganyifu wowote unafanyika katika zoezi hili" Alisema Waziri Dk. Khalid Pamoja na mambo mengine Mhe. Waziri amewataka watendaji wanaosimamia zoezi la fidia kuwa makini katika kazi zao na kuachana na aina yoyote ya hila kwani akiwa msimamizi Mkuu wa waizara hatomvumilia Mtendaji ataekwenda kinyume na maadili ya kazi yake. Nao wananchi wa Shehia hiyo wakiongozwa na Mhe. Sheha wameiomba wizara kufanya tena thathmini kwa kutumia njia sahihi ili kuwatoa watu wasiohusika katika zoezi hilo. Wamesema wapo watu ambao hawahusiki kabisa katika kazi itakayoendelea katika eneo hilo lakini kutokana na kukosa uaminifu hujitokeza na kudai kupatiwa fidia kinyume na utaratibu. Kwa upande wake Naibu waziri Mhe. Nadiri Abdula-TIF akiwa muwakilishi katika jimbo hilo amesema Wananchi wa Kandwi hawana matatizo katika masula yenye maslahi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuwa watatoa ushirikiano unaostahiki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Eng Zena Said anwani ya ofisi ya Rais Ikulu wakati wa kikao kazi na uzinduzi wa operesheni ya anwani za makazi, Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sheikh Abdul Wakil, Zanzibar katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolijia ya Habari, Mhe Nape Nnauye.
Hafla ya utiaji saini baina ya Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupiti Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Kampuni ya Simu ya Zantel iliyoshuhudiwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu wa pande zote mbili (SMT na SMZ) iliyokua na dhumuni la Ujenzi wa Minara ya Simu kwa maeneo ambayo hayana Mawasiliano ya simu Zanzibar.
18-03-2022 16:03:34
22-01-2022 16:01:27